Saturday 22 August 2015

Timberlake afanya kufuru

MWANAMUZIKI Justin Timberlake ameonyesha ujeuri ya pesa baada ya kutoka 'out' na mpenzi kwa ajili ya chakula cha usiku na kutumia takriban Dola 5000.


Kwa mujibu wa jarida la OK, furaha ya kupata mtoto ndio ilimsukuma Timberlake kufanya matumizi makubwa kiasi hicho kumshukuru Jesica Biel.
Inasemekana wawili hao walionekana wakifurahi na kujichana mapochopocho katika hoteli ya Wolfgang ambayo yalipigwa hesabu na kufikia Dola 5000.

No comments:

Post a Comment