Wednesday 19 August 2015

Mwema- Mercy Masika Lyrics


Verse 1
Wako mwana, ukamtuma ,duniani, 
kisa na maana, nipate uzima, jamani 
Ishara kwamba unanipenda zaidi 
ivo nishaelewa, sifa nitakupa zaidi
Chorus
Na siwezi jizuia ,kusema wako wema 
Na sio kama najigamba, umenitenda mema 
Umekua mwema kwangu,

Verse 2
Umanitoa gizani , nilipokuwa nimeshikwa mateka
Ukanipa tumaini, kwako nikajificha
sasa nitakupa nini ,iwe sawa na yale umetenda
Hakuna ila moyoni, sifa nitakuimbia
Ilikugharimu , msalabani unifie
Hivo inanibidi, sifa nikuimbie
Wema wako niseme, ili na wengine wakujue
Wote waungane nami, na wazee ishirini na nne

Chorus
Na siwezi jizuia ,kusema wako wema 
Na sio kama najigamba, umenitenda mema 

Bridge
Umekua mwema kwangu, wachaniringe
Umekua mwema kwangu, ooh yahwe
kwangu,  ooh umenitendea

Na siwezi jizuia ,kusema wako wema 
Na sio kama najigamba, umenitenda mema
Siwezi jizuia

No comments:

Post a Comment