Saturday 22 August 2015

Lupita aacha gumzo mjini

Mara kadhaa ameonekana akiwa na nywele fupi lakini muonekano wake mpya aliotoka nao hivi karibuni umeonekana kuzua mjadala wa aina yake kwenye mitandao ya kijamii.


Ninaye mzungumzia hapa ni nyota wa Hollywood mwenye asili ya Kenya ambaye hivi karibuni alionekana akiwa na nywele bandia kitu  ambacho ni nadra kuonekana kichwani kwake.
Mjadala huo umeibuka baada ya picha kuzagaa kwenye mitandao zikimuonyesha nyota huyu akiwa na muonekano tofauti na ilivyozoeleka. Dada huyo amejizolea umaarufu mkubwa duniani kote baada ya kupata tuzo ya Oscar kufuatia kufanya vizuri katika filamu ya 12 Years a Slave.

No comments:

Post a Comment