Friday 2 October 2015

Uliza Kiatu - H_art the Band Lyrics

Verse 1
You see love, makes you do crazy things
Ask my shoes, uliza kiatu
And what I went through to buy you those rings

Ask my shoes, uliza kiatu
Masaibu ninayoyapitia, kukupeleka dinner
Uliza kiatu
Na gatheri ninavyokatafuna, eti ndo ukule burger, pizza
Uliza kiatu


Chorus
Ask my shoes, ask my shoes
Uliza kiatu, uliza kiatu

Ask my shoes, ask my shoes
Uliza kiatu, uliza kiatu

Verse 2

Nimekopa nikupe, kumbe wewe ndo kupe
Nang'ang'ana ndo tule, juhudi zangu bure
I heard that love should always make us strong
But how I feel like think that they were wrong
Ask me why

Bridge
Nasema taxi nilipe, rent mi nikupe
Nywele zisongwe Mombasa si twende
Mapenzi nikupe, mpaka we uridhike

Nasema taxi nilipe, rent mi nikupe
Nywele zisongwe Mombasa si twende
Mapenzi nikupe, mpaka we uridhike

Chorus

Spoken Word
Kitendawili, kitendawili [tega]
Nilimwonyesha mapenzi akanionyesha mfuko
Alisema doh ya salon ni thao tu
Na kwa mfuko nilikuwa na mbao juu
Alisema anaenda PE
Akirudi nilimpata akimeza P2
[alikutega]
So niko stuck katikati
Kama stick ya mshikaki
Nampenda huyu mshikaji
But kiatu tu ndo inajua stori
Yaani vile, mi humchocha nimemflash bahati mbaya
Ju niko na deni ya bob, Collymore
Yaani vile mi hukanyanga matope kabla nifike kwa lami
Na ile stress mi hupitia kabla nimbongeshe kilami
Yaani vile, mi humpandisha taxi
Then naenda kudandia gari ya moshi
Yaani vile, mi humhustlia hadi kiatu yangu inaanza kutoa moshi
Yaani vile, mi humuita baby
Juu najua nikimuita Njeri
Hiyo r inaeza geuka l
Na hiyo moment naeza kuwa nimeispoil
Yaani vile, nimetarmac hadi
Timber yangu inaeza geuka Sandak
Yaani vile, yaani ka ni kukokwa nimekopa
Yaani ka nikuokoka nimeokoka
Yaani ka ni tisa nimepigana tu
Ndo niivishe hiyo figure yake namba nane
Na hata usiku nipate umenichorea nane
Toa moja, saba
Vile nimesag mpaka toja
Nikamdanganya eti mi naishingi Umoja
Nikwamwonyesha mpaka mi si mwana vi-oja
Eti nawork mahakamani kusolve vitimbi za dunia
Bila shaka mashtaka
Yaani vile hata vile dunia ikasimama tutasimama pamoja
Yaani vile, ka mapenzi ni nywele basi we ulinisetia nati
Yaani vile ka mapenzi ni kikohozi
Basi bila shaka niko na TB, niko na fever juu ananiumiza
Yaani vile, ka mapenzi ni mistari
Basi namwandikia sentensi
Matenzi mpenzi nakuenzi vishenzi
Niko chizi, crazy
Mwizi, wa mapenzi
Nifunge, am guilty
Here to testify

Chorus

No comments:

Post a Comment